Wednesday, March 9, 2011

Mchungaji Mwasapile na Dawa Mugariga (Loliondo)


Muhtasari wa dawa na Tabibu:
  Mgunduzi wa dawa ni Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile (76) anayesema alioteshwa ndotoni na Mungu tangu mwaka 1991 ili aitumie kutibu watu
  Mahali anakopatikana ni eneo la kwa Mchungaji katika Kijiji cha Samunge, Sale, wilayani Ngorongoro, umbali ya takriban kilometa 400 kutoka jijini Arusha.
 Jina la dawa ni "Mugariga" inatokana na mti aina ya mugariga.
  Matumizi yake ni kunywa kikombe kimoja tu, na ni marufuku kurudia.
Gharama yake hadi sasa ni shilingi 500/- tu.

Mchungaji anasema dawa inatibu maradhi sugu kama vile UKIMWI, kisukari, pumu, saratani n.k.
 Watu wamekuwa wakifika Samunge kwa njia mbalimbali, binafsi na hata za kutumia vyombo vya serikali. Wengine hutembea kwa miguu, kukodi magari (kukodi gari kutoka jijini Arusha itakugharimu kati ya shilingi 80,000 na 100,000 il hali mabasi ya kawaida yakitoza kati ya sh. 40,000 na 65,000.), pikipiki, helikopta na magari ya Serikali (kama inavyoonekana pichani).
  Wingi wa watu, kuanzia juzi (Ijumaa) umesababisha askari wa Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakishirikiana na mgambo kuweka ulinzi kulinda usalama na kuhakikisha watu wanapata dawa bila kutokea vurugu.
 Msaidizi wa Mch. Mwasapile, Marko Nedula amesema tayari Askofu wa KKKT jimbo la Arusha, Thomas Lazier aliwatembelea na kuahidi kusaidia upanuzi wa eneo la kutolea dawa.
Changamoto iliyopo:
 Tabibu anasema, "Sasa ninahitaji dawa zaidi ya kuchemsha, maji mengi sana na usafiri wa kufuata dawa nyingi kwa wakati na eneo la kutolea matibabu kwa sababu hapa nilipo hapatoshi kwa umati mkubwa uokuja."... “Naomba Serikali inisaidie kupata usafiri wa vijana kwenda kuleta dawa porini kwani ni nyingi sana, pia vyombo vya kuchemshia dawa na vikombe vya kutolea dawa pamoja na kuboresha barabara ya kuja hapa kwani ni mbaya sana.”
 Wananchi, “Watu wanalala chini, hakuna vyoo, wala hoteli. Pia barabara ya kufika hapa ni mbovu sana. Tunaaomba Serikali itambue mchango wa babu huyu ili asaidiwe watu wengi zaidi kwa urahisi.”
Anthony Mayunga anaripoti kutoka Serengeti kuwa huduma hiyo imeongeza hamasa ya watu kupima afya zao kujua hali zao ili wawahi kupata dawa hiyo... “Wakazi wa Mugumu na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika vituo vya kupimia virusi vya UKIMWI, ili kwenda kupata dawa hiyo wilayani Loliondo..." na mmoja wa wahudumu wa afya katika hospitlia ya Nyerere anaongezea "Watu wanaokuja kupima maamvukizi ya virusi vya UKIMWI wameongeza ghafla. Wengi wao wanasema wanataka kujua kama wameambukiswa VVU wawahi kwa mchungaji kupata dawa.”
Serikali inatamka nini kuhusiana na habari hii?
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Lucy Nkya kupitia mahojiano na Mchungaji huyo katika Televisheni ya Taifa, TBC, anasema - Serikali inafuatilia dawa zake na kwa kuwa ni za miti shamba zitachunguzwa, zikithibitishwa kwamba hazina madhara kwa watumiaji haziwezi kuzuiwa. Naibu Waziri akawaonya wagonjwa wanaopata matibabu ya HIV dhidi ya kuacha kutumia matibabu ya kitalaamu.
 Moses Mashalla anaripoti kutoka Arusha kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Isdori Shirima, ameunga mkono huduma ya mchungaji huyo. Shirima alisema Serikali mkoani Arusha haina tatizo na huduma hiyo maadamu haihatarishi usalama wa raia na mali zao.  “Serikali mkoani Arusha haina tatizo na mchungaji huyo maadamu hahatarishi usalama wa raia na mali zao,”alisema Shirima.

No comments:

Post a Comment