Wednesday, March 9, 2011

Breaking News "Dawa ya Mch Mwasapile wa Loliondo Yazuiwa"

Serikali imetoa tamko Rasmi la Kusitisha Dawa Ya Mugariga Iliyokuwa ikitolewa Na Mch Mwasapile wa Loliondo, Tamko Hilo limetolewa na Waziri wa Afya  Leo hii Jioni.Uchunguzi unaendelea kufanyika ili kujua viwango vya Dawa hiyo......


More updates.........


Update za Nyuma
Wakati maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakiendelea kumiminika katika Kijiji cha Samunge, Ngorongoro mkoani Arusha kupata tiba ya mitishamba inayotolewa na Mch. Ambilikile Mwasapile inayodaiwa kutibu maradhi hatari, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inatuma wataalamu wake kupata ukweli juu ya dawa hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, jana alilithibitishia gazeti la MTANZANIA na kituo cha redio cha BBC Swahili kwa simu kwamba tayari ameiagiza Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ifanye kazi hiyo haraka.

Kadhalika, alisema ameiagiza Taasisi ya Taifa ya Uchunguzi wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ishiriki katika kubaini ukweli juu ya “Dawa ya Maajabu ya Mungu” ambayo Mchungaji Mwasapile anasema ameipata baada ya kuoteshwa na Mungu.

“Nimewaagiza wataalamu waende waone what’s going on, bado hatujapata taarifa rasmi, lakini tunaambiwa maelfu kwa maelfu ya watu wanakwenda huko kutibiwa,” alisema na kuongeza “Lazima tufanye utafiti wa kimaabara kubaini ukweli, isije ikawa ni dawa ya kupooza tu ukali wa ugonjwa, lakini ikawa haitibu. Tutatoa tamkoa rasmi baada ya kupata majibu ya kisayansi ya kimaabara.”

Bi. Blandina alisema uchunguzi wa dawa hiyo utafanywa na majibu yake yakipatikana yatatolewa mapema iwezekanavyo.

2 comments:

  1. We umekuwa wa kwanza kutoa hii breaking news. Mtu angesoma kwako angesave pesa kwa kutokwenda. Blogs zingine zote zimetoa habari hii 'kesho yake' wakati mi naona ni too late. Hongera

    ReplyDelete