Friday, December 23, 2011

Mafuriko yaikumba Dar !

Maji yakiwa yamezingira nyumba na mitaa ya Magomeni maeneo ya Jangwani na kuleta madhara makubwa ya kuharibu makazi ya watu na mali zao na hata kupoteza maisha ya wakazi wa maeneo hayo.

Hao ni baadhi ya wakazi wa maeneo ya Kigogo wakiokolewa na wazamiaji. Unaweza kuona wakina mama na watoto wadogo wakiwa katika harakati za kuokoa maisha yao baada ya maji ya mafuriko kuyakumba maeneo yao.

Hapa ni eneo la daraja la Kawe katika barabara ya Bagamoyo linalounganisha maeneo ya Mbezi na Kawe na Makongo. Daraja hilo lilibomolewa na maji upande mmoja na kusababisha magari kushindwa kupita hapo, pichani wanaonekana wakzi wa maeneo hayo wakitembea kwa miguu kuvuka daraja hilo.

No comments:

Post a Comment